Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera aamini Bocco, Kagere wataibeba Simba mechi za CAF

Fri, 4 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amewataja John Bocco na Meddie Kagere ndio waliobeba siri ya mafanikio ya Simba kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba inatarajia kuanza na JS Saoura mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa Januari 12 mwaka huu baada ya kuingia hatua ya makundi kwa kuitoa Nkana Red Devils ya Zambia kwa jumla ya mabao 4-3.

Akizungumza na Mwananchi, Zahera jana, alisema kwa maana ya uchezaji wa nyota hao wanavyocheza wanaweza wakawa chachu ya mafanikio kwa klabu yao katika hatua ya makundi waliyoingia na kuweka wazi kuwa ni wapambanaji.

“Nawahehimu sana hao wachezaji wanajua kupambana ninatamani kuwa na wachezaji wa namna hiyo katika klabu yangu wanajua nini wanafanya, vimo vyao nguvu na kasi ya kukimbia inaongeza ubora wao wanapokuwa uwanjani,”

Alipoulizwa kuhusu Emmanuel Okwi, Zahera alisema hamfahamu ubora wake isipokuwa wachezaji aliowataja ndio anaokubali viwango vyao na anaamini ndio wanaweza kuibeba timu katika mashindano na kuweka wazi kuwa wakipambana zaidi wanaweza kuitoa kimasomaso timu yao.

“Kuwataja nyota hao sina maana kwamba waliobaki ni wabaya hapana wote ni wazuri lakini wanazidiana, kiujumla Simba ni timu nzuri inawachezaji wengi wenye vipaji kikubwa wnatakiwa kujielewa na kuthamini jezi ya timu wanayoichezea,”



Chanzo: mwananchi.co.tz