Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera: Tunawaombea Simba kutinga robo fainali CAF

45795 Pic+zaher Zahera: Tunawaombea Simba kutinga robo fainali CAF

Mon, 11 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kocha Mkuu wa Yanga amesema maombi yake ni kutamani kuiona Simba ikisonga mbele katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Zahera amesema kuelekea mchezo wa leo usiku Simba wanaweza kufanya vizuri kulingana na ubora wa kikosi chao jinsi kilivyo.

Amesema hata hivyo mechi hiyo haitakuwa nyepesi kwa wawakilishi hao wa nchi na kwamba kitendo cha Saoura kupoteza kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza hapa nchini na kulalamika kutaufanya mchezo huo kuwa mgumu.

 Amesema Yanga inaiombea Simba ifanye vizuri kutokana na itakuwa heshima kwa nchi endapo watani wao hao watasonga mbele.

Ameongeza kuwa endapo Simba itasonga mbele matokeo yake yatakuwa na faida kubwa kwa Soka la Tanzania kwa Klabu nyingi kunufaika na matokeo hayo.

Simba inacheza mechi hiyo leo usiku mjini Bechar Algeria ambapo ikitamani kupata ushindi au sare huku ikiomba dua mbaya katika mchezo utakaotangulia kati ya AS Vita dhidi ya Al Ahly pale Uwanja wa Mashujaa jijini Kinshasa kabla ya mechi za mwisho wakati Simba ikiwakaribisha Vita Club, na Ahly wakiwa wenyeji wa Saoura.



Chanzo: mwananchi.co.tz