Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera, Mwandila watua mikononi mwa bilionea

90286 ZAHERA+PIC Zahera, Mwandila watua mikononi mwa bilionea

Mon, 30 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

UKISEMA cha nini wenzako wanasema watakipata lini. Unaambiwa makocha waliotupiwa virago Jangwani, Mwinyi Zahera na msaidizi wake Noel Mwandila wameungana tena pamoja nchini Zambia baada ya kujiunga na chama analochezea mshambuliaji wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Eliuter Mpepo. Mpepo alijiunga na Buildcon mapema mwaka huu akitokea Singida United, lakini kabla ya hapo alishaichezea Prisons, na alipishana na Lamine Moro aliyejiunga na Yanga na aliyekaribia kutimka akidai malimbikizo ya fedha zake za mishahara na posho kabla ya kutekelezewa. Taarifa za uhakika kutoka Zambia zinasema kuwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Zahera akimalizana na mabosi wa timu hiyo tu kesho yake anatua Zambia katika klabu hiyo ya bilionea mzito lakini msaidizi wake, Mwandila ameshatangulia huko mapema. Bilionea wa klabu ya Buildcon ya Zambia sasa ndoto zake kufanya kazi na kocha Zahera zitatimia wakati wowote mara tu Zahera atakapomalizana na Yanga. Zahera bado yuko nchini akila upepo wa Bahari ya Hindi akisubiri muafaka na Yanga kumalizana juu ya fidia ya kuvunjiwa kwake mkataba, lakini bilionea wa Buildcon, Moses Mubanga amemwambia Mkongomani huyo kwamba asijali ajira katika klabu hiyo ni yake, ila anachotaka ni barua ya kumalizana vyema na Yanga. Bosi mmoja wa Buildcon ameliambia Mwanaspoti kuwa Mubanga ni shabiki mkubwa wa Zahera na kwamba mpaka sasa nafasi ya kocha mkuu haina mtu ikiwa ni nafasi pekee ambayo iko wazi katika benchi la ufundi. “Nafikiri atakuja, wewe fuatilia akimalizana na Yanga nina uhakika atakuja Buildcon, bosi wangu (Mubanga) anampenda sana huyo kocha,” alifichua bosi mmoja wa klabu hiyo. Mapema Zahera kabla ya kutua Yanga aliwahi kufanya kazi katika klabu hiyo kwa wiki chache kabla ya Yanga kumnyakua juu kwa juu wakati akisubiri mkataba. Buildcon tayari ilishamuondoa Kocha Mzambia Tenant Chambo ‘TC’, wakiona hakuwa mtu sahihi katika jukumu hilo ambapo tangu aondolewe kocha wa makipa wa timu hiyo alishikilia nafasi hiyo kwa muda.

UKISEMA cha nini wenzako wanasema watakipata lini. Unaambiwa makocha waliotupiwa virago Jangwani, Mwinyi Zahera na msaidizi wake Noel Mwandila wameungana tena pamoja nchini Zambia baada ya kujiunga na chama analochezea mshambuliaji wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Eliuter Mpepo. Mpepo alijiunga na Buildcon mapema mwaka huu akitokea Singida United, lakini kabla ya hapo alishaichezea Prisons, na alipishana na Lamine Moro aliyejiunga na Yanga na aliyekaribia kutimka akidai malimbikizo ya fedha zake za mishahara na posho kabla ya kutekelezewa. Taarifa za uhakika kutoka Zambia zinasema kuwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Zahera akimalizana na mabosi wa timu hiyo tu kesho yake anatua Zambia katika klabu hiyo ya bilionea mzito lakini msaidizi wake, Mwandila ameshatangulia huko mapema. Bilionea wa klabu ya Buildcon ya Zambia sasa ndoto zake kufanya kazi na kocha Zahera zitatimia wakati wowote mara tu Zahera atakapomalizana na Yanga. Zahera bado yuko nchini akila upepo wa Bahari ya Hindi akisubiri muafaka na Yanga kumalizana juu ya fidia ya kuvunjiwa kwake mkataba, lakini bilionea wa Buildcon, Moses Mubanga amemwambia Mkongomani huyo kwamba asijali ajira katika klabu hiyo ni yake, ila anachotaka ni barua ya kumalizana vyema na Yanga. Bosi mmoja wa Buildcon ameliambia Mwanaspoti kuwa Mubanga ni shabiki mkubwa wa Zahera na kwamba mpaka sasa nafasi ya kocha mkuu haina mtu ikiwa ni nafasi pekee ambayo iko wazi katika benchi la ufundi. “Nafikiri atakuja, wewe fuatilia akimalizana na Yanga nina uhakika atakuja Buildcon, bosi wangu (Mubanga) anampenda sana huyo kocha,” alifichua bosi mmoja wa klabu hiyo. Mapema Zahera kabla ya kutua Yanga aliwahi kufanya kazi katika klabu hiyo kwa wiki chache kabla ya Yanga kumnyakua juu kwa juu wakati akisubiri mkataba. Buildcon tayari ilishamuondoa Kocha Mzambia Tenant Chambo ‘TC’, wakiona hakuwa mtu sahihi katika jukumu hilo ambapo tangu aondolewe kocha wa makipa wa timu hiyo alishikilia nafasi hiyo kwa muda. MWANDILA MAPEMA TU Wakati Zahera akisubiriwa dalili za dili hilo zilizidi kuongezeka baada ya aliyekuwa msaidizi wake ndani ya Yanga, Mwandila kupewa ajira Buildcon. Mwandila amepewa mkataba mzuri akiwa kama kocha msaidizi huku akiambiwa amsubiri bosi wake mpya na tayari jamaa ameshaiongoza timu hiyo kushinda mechi mbili mfululizo. Mwandila, raia wa Zambia ameikuta Buildcon haijashinda katika mechi tano mfululizo tangu walipofanya hivyo Oktoba 24, waliposhinda kwa bao 1-0 dhidi ya Lumwana Radiants. Tayari ameishaipa timu hiyo pointi sita kuanzia mchezo wake wa kwanza ambao walikutana na Mufulira kisha kuichapa Red Arrows. Zahera ambaye ni muumini mkubwa wa Mwandila inaelezwa ndiye aliyemtaka bilionea Mubanga kumchukua msaidizi wake huyo ambapo pia hata akiwa Yanga licha ya uongozi wa klabu hiyo kutaka kumuondoa Mkongomani huyo aligomea uamuzi huo. Mapema jana, Mwanaspoti lilimtafuta Mwandila na kutaka kujua kuanza kazi kwake katika klabu hiyo ambapo alisema anafurahia mwanzo wake mzuri ndani ya Buildcon huku akimtupia mzigo Zahera kueleza safari yake ya kutua klabuni hapo. “Ndiyo, nipo hapa nashukuru nimeanza kazi salama, unapokuta timu haijafanya vizuri kwa muda mrefu ni wazi kuna kuwa na presha lakini sasa imeondoka tumeanza kufanya vizuri,” alisema Mwandila. “Nipo hapa kama kocha msaidizi, hiyo ndiyo nafasi yangu, nimeambiwa kuwa kocha mkuu atakuja wakati wowote. Kuhusu Zahera kama anakuja hapa (anacheka kidogo), nafikiri mtafute mwenyewe atakuambia kama anakuja hapa au vinginevyo.”

Chanzo: mwananchi.co.tz