Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera: Mazembe! Simba wajipange tu

49170 Zahera+pic

Thu, 28 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

JAMAA huwa hapindishi maneno linapokuja suala la kusema ukweli na sasa amefunguka tena hadharani.

Ndio, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameuzungumzia mchezo wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na TP Mazembe utakaochezwa Aprili 6, mwaka huu Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, kuwa lolote linaweza kutokea.

Zahera, ambaye aliingia kwenye mzozo mkubwa na mashabiki wa Simba mechi ya marudiano wakati wanajiandaa kucheza dhidi ya AS Vita hatua ya makundi, akituhumiwa kuwasaidia wageni hao.

Hii ni kutokana na wakereketwa wa Simba kuamini Zahera aliwapa msaada AS Vita kwa sababu ni Wakongo wenzake, lakini hatimaye Wekundu hao wa Msimbazi waliibuka na ushindi na kuingia robo fainali. Simba ilishinda bao 2-1.

“Ninachoweza kusema, mpira wa sasa hauna heshima na hautabiriki. Ile dhana ya kusema timu kubwa ndiyo inaweza kushinda hilo siku hizi hakuna, hata ndogo inaweza kufanya mambo makubwa kitu kikubwa ni kujipanga tu,” alisema Zahera.

Alisema Simba kama itajipanda na kucheza kwa malengo ina nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi bila kujali ukubwa ya TP Mazembe. Pia TP Mazembe ina nafasi ya kufanya vizuri kwa sababu ya maandalizi mazuri.

“Kutokana na hilo timu yoyote inaweza kuibuka na ushindi na kuendelea nusu fainali inaweza akawa Simba au Mazembe,” alisema Zahera.

Simba na TP Mazembe zinacheza mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa hatua ya robo fainali ambapo Simba itaanzia nyumbani na kumalizia ugenini.



Chanzo: mwananchi.co.tz