Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera: Kurushiwa makopo ni kawaida wala haimuumizi kichwa

Video Archive
Tue, 29 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kama ulifikiri Mwinyi Zahera anatishwa na kutupiwa makopo na mashabiki wa Yanga baada ya kufungwa jana basi unajidanganya.

Yanga imefungwa na Pyramids FC mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza na Mwanaspoti, Zahera alisema ajaanza kufundisha soka jana wala juzi hivyo tabia za mashabiki anazifahamu vizuri na yeye kurushiwa makopo ni kawaida wala haimuumizi kichwa.

"Nadhani tukio hili tena kwa Mwanza sio la kwangu mimi tu nilishuhudia kwa kocha wa Simba, Patrick Aussems alivyofungwa na Mbao alirushiwa makopo na kutukanwa, lakini sasa anashangiliwa ni kutokana na matokeo mazuri anayopata," alisema Zahera.

"Mashabiki hawana maana kuna muda wanakupenda na muda mwingine wanakuchukia hivyo hicho kilichonitokea hakinipi sababu ya mimi kuyumba nitaendelea kukubaliana na changamoto hizo nikiwa kama mwalimu siwezi kutishwa na mashabiki hao leo wanakutukana kesho wanakushangilia nachukulia kama moja ya changamoto," alisema.

Zahera aliongeza kuwa mpira hasa ukanda wa Afrika hakuishiwi matukio kama hayo hivyo itakuwa ni ajabu kwake kama ataamua kuachana na timu kisa kutupiwa makopo na mashabiki na kusisitiza kuwa yeye ni kopcha wa kuajiliwa hivyo ataendelea kubaki Yanga.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz