Cairo, Misri. Bao la mshambuliaji nyota wa Crystal Palace Wilfried Zaha limeipeleka Ivory Coast robo fainali ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).
Zaha alifunga bao hilo dakika ya 76 kwa kiki ya karibu na kuipa ushindi wa bao 1-0 Ivory Coast dhidi Mali jana usiku.
Nyota huyo anayehusishwa na mpango wa kutua Arsenal katika usajili wa majira ya kiangazi, alifunga bao hilo akiwa karibu na kipa wa Mali Djigui Diarra.
Mali iliyotawala mchezo, ilikosa nafasi za kufunga kupitia kwa wachezaji Moussa Marega na Moussa Djenepo ambao walishindwa kuweka mpira wavuni licha ya kuwa eneo zuri.
Ivory Coast iliyotwaa ubingwa wa Afrika mwaka 1992 na 2015, haikuwa katika kiwango bora kulinganisha na Mali iliyocheza soka ya kuvutia.
Timu hiyo yenye idadi kubwa ya nyota wanaocheza ligi maarufu Ulaya ilicheza chini ya kiwango hasa kipindi cha kwanza cha mchezo huO.
Pia Soma
- Maji ya Dk Kijaji kunusuru ndoa
- UCHOKOZI WA EDO: Kumuona Kenyatta mara kwa mara inafurahisha
- Picha kamili ya kesi inayomkabili Harry Kitilya na wenzake
Pia kiki ya Abdoulay Diaby ilipanguliwa na kipa wa Ivory Coast kabla ya Djenepo kupoteza nafasi nyingine ya kufunga.
Katika mchezo mwingine, Tunisia ilifuzu robo fainali kwa ushindi wa mabao 5-4 iliyopata dhidi ya Ghana kwa penalti, baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 120.