Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ZBC MAPINDUZI CUP KUANZA RASMINI DESEMBA 18

Capture 574?fit=436%2C345 ZBC MAPINDUZI CUP KUANZA RASMINI DESEMBA 18

Wed, 16 Dec 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana Sanaa na Utamaduni na Michezo Zanzibar Omar Hassan (King) amesema kuwa mashindano ya ZBC Mapinduzi Cup ya Watoto yanatarajiwa kuanza siku ya Ijumaa ya 18 Disemba.

Mashindano mengine ni ya Mawizara na Taasisi za Serikali za Zanzibar na Taasisi za Serikali za Tanzania Bara zinazofanyia kazi zake hapa Zanzibar na mengine yatakuwa ni mashindano ya Wanawake ambayo hayo yanasimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar ZFF.

Ni mfululizo wa alichokiongea Katibu huyo Omar Hassan King wakati alipokua akizungumza na Waandishi wa Habari za Michezo kuhusu Mashindano ya Kombe hilo akiwa huko Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Jijini Zanzibar.

Chanzo: zanzibar24.co.tz