Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yondani avuta beki mpya Yanga SC

84811 Yondan+pic Yondani avuta beki mpya Yanga SC

Tue, 19 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. KIKOSI cha Taifa Stars kipo jijini Tunis, Tunisia tayari kwa maandalizi ya mwisho kukutana na wapinzani wao Libya, lakini huku nyumbani hasa pale Jangwani  beki wao mmoja amekaribia kulazimisha usajili mmoja muhimu. Yanga wameifuatilia Stars ikicheza dhidi ya Guinea ya Ikweta juzi Ijumaa usiku na kushinda 2-1 lakini utulivu waliouonyesha beki wao Kelvin Yondani na Bakari Mwamnyeto ‘Nondo’ ghafla ukainua mjadala mfupi ambao maazimio ni kuhakikisha beki huyo anatua Jangwani fasta. Mabosi wa Yanga ambao wako katika Kamati ya Ufundi ya Yanga ambayo kwa sasa usajili wa timu hiyo kwa kiasi kikubwa utapitia hapo wamemwangalia Mwamnyeto kwa jicho la tatu na kuona anaweza kuja kuwa beki muhimu baadaye. Katika kikao hicho mabosi hao walikubaliana Mwamnyeto akiwa na timu yake ya Coastal Union huwa hana ubora mkubwa, lakini anapokuja kucheza na mkongwe yeyote hasa akiwa Taifa Stars anakuwa hatari zaidi na hapo ndipo ikaamuliwa lazima asajiliwe Yanga. Kucheza kwake na Yondani kisha kuonyesha uwezo mkubwa akiwa na mkongwe huyo ndio kumewafanya mabosi hao kuchukua jina lake na kulipelekia mbele ya uongozi wao tayari kwa kufanyiwa kazi kiusajili, ili aje kutengeneza ukuta wa chuma Jangwani.

Dar es Salaam. KIKOSI cha Taifa Stars kipo jijini Tunis, Tunisia tayari kwa maandalizi ya mwisho kukutana na wapinzani wao Libya, lakini huku nyumbani hasa pale Jangwani  beki wao mmoja amekaribia kulazimisha usajili mmoja muhimu. Yanga wameifuatilia Stars ikicheza dhidi ya Guinea ya Ikweta juzi Ijumaa usiku na kushinda 2-1 lakini utulivu waliouonyesha beki wao Kelvin Yondani na Bakari Mwamnyeto ‘Nondo’ ghafla ukainua mjadala mfupi ambao maazimio ni kuhakikisha beki huyo anatua Jangwani fasta. Mabosi wa Yanga ambao wako katika Kamati ya Ufundi ya Yanga ambayo kwa sasa usajili wa timu hiyo kwa kiasi kikubwa utapitia hapo wamemwangalia Mwamnyeto kwa jicho la tatu na kuona anaweza kuja kuwa beki muhimu baadaye. Katika kikao hicho mabosi hao walikubaliana Mwamnyeto akiwa na timu yake ya Coastal Union huwa hana ubora mkubwa, lakini anapokuja kucheza na mkongwe yeyote hasa akiwa Taifa Stars anakuwa hatari zaidi na hapo ndipo ikaamuliwa lazima asajiliwe Yanga. Kucheza kwake na Yondani kisha kuonyesha uwezo mkubwa akiwa na mkongwe huyo ndio kumewafanya mabosi hao kuchukua jina lake na kulipelekia mbele ya uongozi wao tayari kwa kufanyiwa kazi kiusajili, ili aje kutengeneza ukuta wa chuma Jangwani. Kumbe Mwarabu alimtibulia Wakati mabosi hao wakijadiliana, hivyo Mwanaspoti linafahamu kuwa Mwamnyeto alitakiwa muda mrefu kusajiliwa na Yanga, lakini baadhi hasa mabosi wa juu wa klabu hiyo wakauzuia usajili wake ili achukuliwe Ali Ali ‘Mwarabu’ aliyekuwa KMC. Hatua hiyo ya kumpotezea Mwamnyeto na kumchukua Mwarabu, ilitokana na kubaini beki huyo aliyewahi kuichezea Stand United mbali na kumudu kucheza kama beki wa kati pia angeweza kucheza kama beki wa kulia lakini haikuwa hivyo. “Kupelekwa kwa jina la Mwamnyetoni mara ya pili unajua hizi timu zetu zina shida sana, dirisha kubwa la usajili alipendekezwa lakini kuna mmoja wetu mwenye nguvu akasema asajiliwe Ali Aliy kwa kuwa ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi lakini sasa nadhani wanaona na kuelewa tunachosema,” alisema bosi mmoja. Hata hivyo mbali na mabadiliko hayo pia kiasi ambacho klabu yake ya Coastal Union ilikihitaji nacho kilichangia kwa Yanga kurudi nyuma na walihitaji kiasi kisichopungua Sh25 milioni huku Yanga wakitaka kutoa Sh20-15 milioni. Lakini kwa namna mabosi wa Yanga wanavyomhitaji beki huyo huenda mchakato wake ukafanyika haraka mara baada ya beki huyo kurejea kutoka Tunisia kutokana na mabosi hao kukata kukwepa vurugu za beki huyo kupanda bei pale dirisha dogo litakapofunguliwa Desemba 16 mwaka huu. Dirisha hilo la usajili litafungwa Januari 15 mwakani hii ikiwa ni tofauti na ilivyokuwa imezoeleka awali huwa linafunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15 ya kila mwaka, ikitokana na mabadiliko ya kalenda ya michuano ya kimataifa ikitaka kulingana na dirisha la usajili la FIFA.

Chanzo: mwananchi.co.tz