Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yondani akaa jukwaani Yanga ikijiwinda kuivaa Kagera Sugar

51324 Pic+yondani

Wed, 10 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Beki Kelvin Yondani ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake leo wakati Yanga ikijiandaa na mechi ijayo dhidi ya Kagera Sugar.

Katika mazoezi hayo, Yondani akiishia kukaa jukwaani akiuguza majeraha aliyoyapata jana wakati wa mechi yao na African Lyon waliyoshinda 2-0.

Yanga inatarajia kushuka uwanjani Alhamisi kuwakaribisha Kagera Sugar 'Wanakurukumbi' mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Kirumba Mwanza, ukiwa wa raundi ya 31 kwa timu hiyo.

Yanga inaongoza Ligi Kuu ikiwa na pointi 71, huku Kagera Sugar wakiwa nafasi ya 15 kwa pointi 36, hivyo kufanya mchezo huo unatarajia kuwa na ushindani mkali katika vita ya kuwania pointi tatu muhimu.

Mabingwa hao wa zamani wanawakaribisba wapinzani hao wakiwa na rekodi nzuri ya kuwafumua mabao 2-1 katika mechi ya mzunguko wa kwanza uliopigwa mjini Bukoba.

Katika mazoezi hayo Yanga chini ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera wachezaji walikuwa wakichengana, kukabana na kufunga mabao, huku makipa Ramadhan Kabwili na Klaus Kindoki wakipeana zamu golini.

Mazoezi hayo yalidumu kwa takribani saa moja na robo, huku Makomandoo wa timu hiyo wakiwa makini kutoruhusu mashabiki kuingia uwanjani.



Chanzo: mwananchi.co.tz