Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaweka kiporo cha mgogoro

73f0380e97d5d30c60df6fbe60bb341e Yanga yaweka kiporo cha mgogoro

Fri, 24 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KLABU ya Yanga imegoma kuzungumzia mgawanyiko uliojitokeza kwenye benchi la ufundi ndani ya kikosi hicho na kudai kwa sasa mawazo yao wameelekeza kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya Lipuli unaotarajiwa kufanyika Jumapili katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa.

Ndani ya benchi hilo kocha mkuu wa kikosi hicho, Lucy Eymael aligoma kufanya kazi na wasaidi wake, Charles Mkwasa na Peter Manyika kwa madai kwamba wanamuhujumu timu ifanye vibaya ili aachishwe kazi.

Akizungumza kutoka Morogoro jana Ofisa Habari wa kikosi hicho, Hassani Bumbuli aligoma kuelezea mgawanyiko huo kwa kudai kwamba kwa sasa wanaangalia mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara keshokutwa dhidi ya Lipuli. Alisema kuwa suala hilo la mgogoro ndani ya benchi lao la ufundi watalizungumza watakaporejea jijijini Dar es Salaam baada ya mchezo huo wa Iringa.

“Tukianza kuzungumzia suala la mgogoro wakati mbeleni tuna mchezo sio jambo zuri, kikubwa tumeshasema suala hili tutakuja kuliweka bayana baada ya kumaliza kazi kwenye mchezo wetu dhidi ya Lipuli tupate ushindi katika mbio zetu za kuwania nafasi ya pili, “alisema Bumbuli Mkwasa na Manyika hawakuwemo katika benchi wakati Yanga ilkicheza dhidi ya Mtibwa Sugar na kutoka sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, na hawatakuwepo katika mchezo huo wa mwisho.

Hata hivyo, Mkwasa alipozungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu suala hilo, alisema kuwa hakuwepo Morogoro kutokana na matatizo ya kifamilia. Aidha, Bumbuli alisema leo asubuhi kikosi hicho kinarajiwa kuanza safari ya kwenda mkoani Iringa. Eymael alitamba kuibuka na ushindi katika mchezo huo ili kuzidi kujitengenezea mazingira ya kumaliza ligi katika nafasi ya pili.

Chanzo: habarileo.co.tz