Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yawaza pointi 12 Bara

JUMA MWAMBUSI Yanga yawaza pointi 12 Bara

Fri, 2 Apr 2021 Chanzo: ippmedia.com

Yanga ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 50, na ratiba inaonyesha wataendelea na kampeni ya kusaka ubingwa kwa kucheza dhidi ya KMC FC ifikapo Aprili 10 halafu Aprili 17 watawakaribisha Biashara United huku Aprili 24 wakiivaa Gwambina na watamaliza mwezi kwa kuikabili Azam FC Aprili 25, mwaka huu.

Akizungumza na gazeti hili jijini jana, Mwambusi alisema wanaendelea kufanya mazoezi ili kuhakikisha wanajiweka katika nafasi nzuri ya 'kuchanga karata' zao vizuri na hatimaye kukusanya pointi 12 za awali.

Mwambusi alisema ana matumaini makubwa watafanya vyema kwa sababu kikosi chao kimekamilika baada ya wachezaji wao waliokuwa majeruhi akiwamo Saidi Ntibanzonkiza na Fiston Abdul Razack afya zao kuimarika.

"Hali ya kikosi kilichokuwapo kambini kipo sawa kwa wachezaji waliosalia kambini huku bado Saido na Mukoko Tonombe ambao watarejea mapema wakitokea kwenye majukumu ya timu zao za taifa, tunaendelea na programu ili kuhakikisha tunafikia malengo kwa kuanza kukusanya pointi kwenye mechi hizi nne za mwezi huu," alisema Mwambusi.

Aliongeza baada ya nyota hao kurejea kikosi chake kitaendelea kupambana ili kutoa 'dozi' katika kila mechi watakayocheza ingawa wanafahamu kila mchezo utakuwa na ushindani.

"Kuhusu ubingwa tuna nafasi kubwa sana, kikubwa wachezaji kutuliza akili na kufanya majukumu yao ili kutafuta ushindi katika hiyo michezo yote minne ambayo tutacheza nyumbani," alisema Mwambusi.

Aliongeza wanajipanga pia kufanya vizuri katika mchezo wao wa hatua ya 16 Bora wa mashindano ya Kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga, Rukwa.

Chanzo: ippmedia.com