Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatua, akili zote kwa Mbao na Pyramid

80884 Pic+yanga Yanga yatua, akili zote kwa Mbao na Pyramid

Mon, 21 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KLABU ya Yanga leo Jumamosi asubuhi imetua jijini hapa tayari kwa mechi zake mbili za Ligi Kuu na ya Kombe la Shirikisho zitakazopigwa Uwanja wa CCM Kirumba. Yanga inatarajia kushuka uwanjani Oktoba 22 kumenyana na Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu kisha Oktoba 27 kucheza na Pyramid ya Misri ikiwa ni mechi ya kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Akizungumza baada ya kuwasili jijini hapa, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera amesema wamekuja na kikosi cha wachezaji 27 huku wengine wawili walioko timu Taifa 'Taifa Stars', Metacha Mnata na Abdulaziz Makame wakatarajia kuungana na wenzake kesho Jumapili. Amesema leo timu itaanza mazoezi saa 6 mchana uwanja wa Nyamagana huku akifafanua kuwa wamekuja kwa tahadhari kubwa. Amesema wachezaji wote wako fiti hivyo anatarajia watafanya vizuri katika mechi hiyo ya kwanza dhidi ya Mbao FC. Kikosi hicho kimewasili saa 1:45 asubuhi na kupokelewa na idadi ndogo ya mashabiki wake.

Chanzo: mwananchi.co.tz