Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatazama ilipojikwaa mara 3

27150 Pic+yanga+2 Yanga yatazama ilipojikwaa mara 3

Mon, 11 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAKAMU Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, amesema licha ya kutojua Ligi Kuu Bara itarejea au laa, wao wameshaanza mikakati ya kuboresha walipokosea hali iliyosababisha kukosa ubingwa kwa msimu mitatu mfululizo.

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Mwakalebela alisema mbali na usajili ambao watakaoufanya pia kuna mikakati waliyojiwekea kuona kikosi chao kinafikia malengo yanayotarajiwa.

Alisema kukosa ubingwa kwa misimu mitatu kumewafanya kuanza kujipanga mapema ikiwamo upande wa usajili pamoja kuweka mazingira mazuri ya timu yao kujiandaa kwa msimu ujao.

"Katika usajili tunaenda vizuri, mwalimu Luc Eymael ametoa mapendekezo yake na kufanyiwa kazi, lakini viongozi tunaangalia upungufu mwingine na utawala kufanyia kazi," alisema Mwakalebela.

Alisema kwa sasa wanaomba Mungu janga hili la corona liishe, na endapo ligi itarejea wamalize salama na kuendelea na mchakato wao kujipanga kwa msimu ujao.

Mwakalebela alisema muda huu wa likizo ya corona wanautumia kutafakari jinsi gani ya kufikia malengo yao kuhakikisha msimu ujao wanatwaa ubingwa.

Hadi ligi hiyo inasimama Yanga ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 51, ikizidiwa alama 20 na mabingwa watetezi, Simba walioko kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, huku Azam FC ikishika nafasi ya pili kwa pointi zao 54.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live