Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatangulia fainali

138820bba56a9d4adc1ad0bbe5ede37d Yanga yatangulia fainali

Sat, 26 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

YANGA imetangulia fainali baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Biashara United mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) uliochezwa Juni 25 katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Yacouba Songne ndiye shujaa wa mchezo huo aliyewafungia Yanga bao pekee dakika ya 22 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Feisal Salum.

Yanga sasa inamsubiri mshindi wa mechi kati ya Simba na Azam FC katika mchezo wa nusu fainali ya pili utakaochezwa Juni 26 kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea mkoani Ruvuma.

Hii ni mara ya pili Yanga inaingia fainali baada ya msimu wa 2015/16 kuingia na kuchukua kombe hilo. Awali, mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi Kuu walipata bao hilo mapema lililodumu hadi kumalizika kwa mchezo.

Timu hizo ziligawana zamu za kushambulia Yanga ilimiliki mpira kipindi cha kwanza na kupata bao lakini kipindi cha pili Biashara United ilirudi kivingine kwa kushambulia na kutengeneza nafasi nyingi ila ilikosa ufanisi katika umaliziaji.

Kadhalika Yanga, ilitengeneza nafasi kipindi hicho cha pili lakini hawakuwa makini katika umaliziaji na wapinzani wao wakionekana kuwa makini kuwadhibiti.

Timu hiyo ya mitaa ya Twiga na Jangwani Kariakoo ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Deus Kaseke, Yacouba Songne na Tuisila Kisinda na kuingia Saido Ntibazonkiza, Waziri Junior na Paul Godfrey lakini hayakusaidia kuzaa matunda.

Pia, Biashara United iliwatoa Ally Mussa, Ramadhan Chombo na kuingia Christian Sigah na Kelvin Friday ambayo bado hayakusaidia kubadilisha matokeo.

Michuano hiyo ni maalum kwa ajili ya kutafuta wawakilishi wa nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo: www.habarileo.co.tz