Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yasaka makali Mtwara

Yaanga Ed.jpeg Yanga yasaka makali Mtwara

Thu, 13 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo imesema uamuzi wa kuweka kambi Mtwara umetokana na mapendekezo yaliyotolewa na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nassredine Nabi ambaye alihitaji sehemu yenye utulivu zaidi.

"Tumefika Mtwara salama, Kocha Mkuu amehitaji kukaa mjini hapa kwa siku mbili ili  kuendelea na programu yake, na Ijumaa ndio tutakwenda Lindi," kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho kiliongeza wakiwa Mtwara wanahitaji kujiimarisha ili kusaka matokeo chanya katika mechi hiyo ya kiporo ambayo wanahitaji ushindi na kuendelea na mbio za kuwania taji la ubingwa wa msimu huu.

“Kocha Nabi amepata taarifa za nyuma kuhusu wapinzani wetu, ndio sababu ametaka kupata nafasi ya kuandaa timu yake vyema ikiwamo kufanya mazungumzo maalumu na wachezaji ambayo yatajenga kisaikolojia, lakini kuwaandaa kimbinu.”

“Namungo ni timu imara, hatutawabeza wapinzani wetu, tunaimani mchezo huo hautakuwa rahisi kwa sababu ya maandalizi na kikosi tulichonacho pamoja na mbinu za kocha, kikubwa ambacho tunahitaji kupata ni matokeo chanya,” aliongeza.

Alisema wachezaji wako tayari kupambana na kutafuta ushindi dhidi ya Namungo FC, licha ya timu hiyo kuonyesha ushindani katika kila mechi wanayokutana.

“Namungo FC wamekuwa wagumu sana kwetu tangu wamepanda Ligi Kuu, imekuwa ikitusumbua nyumbani na ugenini, sasa tumejipanga vizuri kwa ajili ya kutafuta pointi tatu katika mchezo huo,” aliongeza kiongozi huyo.

Yanga itashuka uwanjani keshokutwa ikiwa na kumbukumbu ya sare ya bao 1-1 waliyopata dhidi ya wenyeji wao kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Chanzo: ippmedia.com