Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yapelekwa tena kwa Alliance Kombe la FA

45207 Ratiba+FA+pic Yanga yapelekwa tena kwa Alliance Kombe la FA

Fri, 8 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wiki moja baada ya kukutana kwenye mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, timu za Yanga na Alliance zitakutana tena kwenye uwanja huo katika mechi ya hatua ya robo fainali ya mashindano ya Azam Sports Federation Cup.

Katika droo ya mashindano hayo iliyochezeshwa asubuhi hii, Alliance imepangwa kucheza nyumbani dhidi ya Yanga.

Kama ilivyo kwa Yanga ambayo itacheza ugenini, Azam FC nayo imepangwa kucheza ugenini kwenye Uwanja wa Kaitaba dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo mwingine wa robo fainali. Mechi nyingine ya robo fainali itahusisha KMC dhidi ya African Lyon wakati Lipuli FC itaialika Singida United.



Chanzo: mwananchi.co.tz