Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yanasa mbadala wa Morisson

E98d2ac7b07e346993365b83513c7bb1.png Yanga yanasa mbadala wa Morisson

Wed, 19 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KLABU ya Yanga imesema inatarajia kumsajili Carlos do Carmo ‘Carlinhos’ kuziba nafasi ya kiungo, Bernard Morrison aliyesajiliwa na Simba.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa GSM ambao ni wadhamini wao, Hersi Said na kusema baada ya kukamilisha usajili wa wachezaji Mukoko Tonombe na Tuisila Kisinda kutoka AS Vita Club ya DR Congo sasa wanahamia kwa washambuliaji.

Alisema baada ya kumleta Carlinhos wanatarajia kumleta mshambuliaji ambaye aligoma kumtaja jina lake kwa sababu bado hawajafanya mazungumzo na timu anayoichezea ili kujiunga na Yanga kwa msimu ujao.

“ Tunatarajia kumaliza usajili wa Carlinhos, raia wa Angola anayekuja kuziba nafasi ya Morrison na mwingine siwezi kumtaja kwa kuwa bado ana mkataba na timu yake na hatujakamilisha mazungumzo, tuwe na subira,“ alisema Said.

Alisema mara baada ya kukamilisha usajili, watamtangaza mchezaji huyo na watasaidia kuunda kikosi kitakachotoa ushindani kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano mengine.

Pia alisema wanatarajia kumtangaza kocha mkuu kesho au kesho kutwa kama mazungumzo yao yanayoelekea mwishoni yatakwenda sawa na kukubaliana.

Chanzo: habarileo.co.tz