Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yamtimua Kocha Eymael

011087f3327694d12fba417b93d05a3f Yanga yamtimua Kocha Eymael

Mon, 27 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KLABU ya Yanga imemfuta kazi Kocha wake, Luc Eymael kutokana na kutoa kauli zisizokuwa zi kiuungwana pamoja na maneno ya kibaguzi ambayo amekuwa akiyaeneza kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari mbalimbali.

Taarifa ya Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Simon Patrick ilisema kuwa kutokana na kauli hizo zisizokuwa za kiuungana, uongozi umeamua kumfuta kazi kuanzia leo Julai 27, 2020 na hata kuhakikisha anaondoka nchi haraka iwezekanavyo.

Patrick alisema kuwa klabu inaomba radhi viongozi wa nchi, Shirikisho la Soka nchini (TFF), wanachama na mashabiki wa Yanga kutokana na kauli za kuudhi na kudhalilisha zilizotolewa na Kocha Eymael.

Chanzo: habarileo.co.tz