Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yamrudisha Yondani kikosini

42168 Pic+yondani Yanga yamrudisha Yondani kikosini

Mon, 18 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Benchi la ufundi la Yanga limemrudisha kikosi cha kwanza beki Kelvin Yondani katika mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania aliingia kutokea benchi.

Beki huyo pamoja na mwenzake Andrew Vincent wamekuwa hawachezi pamoja katika mechi za Yanga za hivi karibuni, lakini leo wameanza pamoja kwenye kikosi cha kwanza.

Mrisho Ngassa ambaye mchezo wa kwanza baina ya timu hizo mwaka jana alikosekana kwenye kikosi cha kwanza, ameanzia benchi kwa mara nyingine leo.

Kikosi cha Yanga kinachoanza leo kipa Ramadhani Kabwili atakayesaidiwa na mabeki Yondani, Andrew Vincent, Gadiel Michael na Paul Godfrey 'Boxer'

Viungo ni Ibrahim Ajibu, Feisal Salum, Papy Tshishimbi na Abdallah Shaibu 'Ninja' wakati washambuliaji ni Amissi Tambwe na Heritier Makambo.

Wachezaji watakaokuwa benchi ni Klausi Kindoki, Juma Abdul, Mateo Anthony, Said Juma, Mrisho Ngassa, Haruna Moshi na Mohammed Issah



Chanzo: mwananchi.co.tz