Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yalia na Waamuzi Kagame Cup

F1c43903dd287773bce48074f61cb150.jpeg Razak Siwa, Kocha wa Makipa Yanga SC

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kocha wa walinda mlango wa Yanga SC, Razak Siwa amewajia juu waamuzi wa michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea Dar es Salaam kwa madai wanaionea timu yake.

Siwa amewataka waamuzi wa michuano hiyo kufuata sheria 17 za soka, huku akiisisitiza Cecafa kuwa makini na upangaji wa waamuzi ili watende haki.

Siwa ambaye kwa sasa ni Kocha wa Yanga katika michuabo hiyo baada ya kocha mkuu, Nasreddine Nabi kwenda kwao Tunisia kwa mapumziko, alisema timu yake ilistahili ushindi katika mchezo wa juzi usiku.

Malalamiko ya kocha huyo yamekuja baada ya kushuhudia kikosi chake kikilazimishwa sare ya bila kufungana na timu ya Atlabara FC katika mchezo wa pili wa Kundi A, ambao ulipigwa juzi Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akizungumza baada ya mchezo huo kumalizika, Siwa alisema timu yake ilistaili ushindi kutokana na kuutawala mchezo kwa dakika zote 90, lakini mwamuzi wa mchezo huo aliwanyonga kutokana na kushindwa kutoa adhabu ambazo walistaili kupewa.

“Timu yangu ilicheza vizuri lakini sikufurahishwa na maamuzi ya mwamuzi sababu ametunyima penalti tano tena za wazi kabisa, hili si jambo zuri sababu klabu imetumia gharama kubwa kuiandaa timu halafu mtu mmoja anakwenda kufanya vitu vya hivyo.”

Kocha huyo alisema katika mchezo wao wa ufunguzi mambo kama hayo yalitokea kwa mwamuzi, lakini wakachukulia kama ni makosa ya kibinadamu, lakini ameshangazwa kuona jambo hilo likijitokeza tena kwenye mchezo wao wa pili.

Siwa alisema wanaona fahari kushiriki michuano hiyo, lakini ipo haja ya waandaaji Cecafa kuwa makini katika uteuzi wa waamuzi wanaochezesha michuano hiyo ili kuondoa malalamiko ambayo yanaharibu maana halisi ya michuano hiyo.

Matokeo hayo yanailazimu Yanga iliyopo nafasi ya tatu na pointi mbili kuifunga Express watakapokutana katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo kesho ili kufikisha pointi tano, huku ikiiombea mabaya Nyasa Bullets kutoa angalau sare na Atlabara ili waweze kutinga hatua nusu fainali.

Chanzo: www.habarileo.co.tz