Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yalamba dili la Sh41 bilioni

Mkataba Pic Data Yanga yalamba dili la Sh41 bilioni

Thu, 8 Jul 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

UONGOZI wa klabu ya Yanga leo Julai 8, 2021 umeingia makubaliano na Azam Media ya kurusha maudhui ya klabu hiyo yenye thamani ya Sh41 milioni pamoja na kodi. Makubaliano hayo ni ya miaka 10 ambayo yatakuwa na tija kwa pande zote mbili. Kaimu katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa amesema mkataba huo ni wa aina yake kwani utakuwa na manufaa zaidi kwao na Azam Media pia.

Amesema kwa kuanzia hii leo baada ya kusaini mkataba huo mnono wataanza na Sh2.4 bilioni. Mfikirwa amesema mkataba huo ni mkubwa kuendana na hadhi ya klabu yao hivyo ambao utazidi kuleta watu.

"Huu udhamini sio mchezo ni wa aina yake na ni wa kihistoria hapa Nchini, " Mfikirwa amesema udhamini huo itakuwa na marejeo Baada ya miaka mitano "Hapo awali tulikuwa na mkataba Kama huu lakini haukuwa mnono sana huu umekuwa mkubwa zaidi,"

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando  amesema lengo lao ni kuhakikisha soka linazidi kukua na kupiga hatua zaidi.

Aidha Tido amesema watakuwa na mambo mengi yanayohusu Yanga ambayo wao ndio watakuwa na haki ya kuyarusha.

"Ushirikiano huu unatuoa nafasi sisi Yanga kurusha kila kitu kinachohusu Yanga kupitia Azam iwe mazoezi, makala za wachezaji na mambo mengine, " amesema Tido.

Aidha Tido amesema Mkataba huo wa miaka 10 utakuwa na thamani ya Sh41 bilioni pamoja na kodi.

Amesema malipo haya yatafanyika kwa msimu na yatalipwa kila mwezi. Msimu huu Sh200 milioni kila mwezi mwezi na baada ya msimu huu kumalizika  msimu ujao itaongezeka na kuwa Sh220 milioni.

Aidha Tido amesema wanatarajia kufanya mazungumzo na Klabu nyingine ambazo zinamvuto kibiashara Kama ulivyokuwa Yanga.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz