Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yajipigia JKT Tanzania yakaa kileleni

29478 Yanga+pic TanzaniaWeb

Fri, 30 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mabingwa mara 27 wa Ligi Kuu Bara, Yanga imepanda kileleni mwa ligi baada ya kuichakaza JKT Tanzania kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga ilipata mabao yake yaliyofungwa na Herities Makambo, Mrisho Ngassa na bao la penalti ya Ibrahimu Ajibu yalitosha kuwafanya mashabiki wa Yanga kusahau shida na matatizo ya fedha yanayoikabili klabu hiyo kwa sasa.

Ushindi huo unaifanya Yanga kuongoza Ligi Kuu ikiwa na pointi 35 baada ya kucheza mechi 13, wakifuatiwa na Azam (33) na Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi 27.

Katika mchezo huyo JKT Tanzania ilitawala sehemu kubwa ya mchezo huo, lakini makosa yao madogo na kukosa uzoefu wa Ligi Kuu ilikuwa faraja kwa Yanga kutumia nafasi chake walizopata kufunga mabao.

Yanga ilipata bao la kwanza dakika 20, baada ya kiungo wa JKT Tanzania, Aziz Gilla kurudisha pasi ndefu ya nyuma ilimkuta Makambo aliyekimbia kwa kasi kabla ya kupiga shuti lililomshinda kipa Abdalrahim Mohammed na kujaa wavuni.

Bao hilo liliwaamsha JKT Tanzania kwani dakika 23 Abdulrahman Mussa alipiga shuti akiwa ndani ya boksi lakini kipa wa Yanga, Ramadhan Kabwili aliucheza mpira huo na kutoka nje.

Dakika 31, Haji Mwinyi alipiga pasi ndefu kwa Ibrahim Ajib, ambaye aliweza kuukimbilia mpira na kisha kumpiga chenga beki Anuary Kilemile na kuingia ndani ya boksi lakini hata hivyo alifanyiwa madhambi na kuanguka chini hata hivyo refa Emmanuel Mwandembwa hakufanya uamuzi wowote.

Kiungo cha Yanga kulikuwa na maelewano mazuri kati ya Feisal Salum na Raphael Daud kwani, Fei alikuwa anakaba na akimuacha Daud akizunguka na kupiga pasi hali iliyomfanya Mwinyi Kazimoto ashindwe kutamba katika dimba hilo la kati.

Katika kipindi cha pili Yanga iliendelea kulisakama lango la JKT Tanzania na dakika 52 Mrisho Ngassa aliifungia timu yake bao la pili na kushangilia kwa mtindo wa kudondoka chini.

Dakika 61, JKT Tanzania walifanya mabadiliko kwa kumtoa Daniel Mecha na kuingia Kelvin Nashon, dakika 66 alitoka Said Luyaya na kuingia Iddy Mbaga.

Yanga walifanya mabadiliko dakika 72 kwa kumtoa Raphael Daud na kuingia Thaban Kamusoko.

Kuingia kwa Kamusoko kulikuwa ni faida kwa Yanga katika dakika 72, aliekewa pasi safi za Makambo ambalo alikwenda kupiga shuti na beki wa JKT Tanzania aliushika akiwa ndani ya boksi na mwamuzi Mwandembwa aliamuru kuwa ni penalti.

Ajibu alipiga penalti hiyo na kuikwamisha nyavuni na kuiandikia Yanga bao la tatu.

Yanga walifanya tena mabadiliko dakika 85 kwa kumtoa Ngassa na kuingia Cleofas Sospeter.



Chanzo: mwananchi.co.tz