Dar es Salaam. Tmu ya Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa leo Jumanne Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la Yanga lilifungwa na kiungo wa Yanga,Papy Kabamba Tshishimbi dakika ya 15 baada ya kutengewa pasi nzuri na Deus Kaseke lilitosha kuamsha ari ya mchezo kwa timu hiyo, tofauti na dakika 10 za mwanzo wa mchezo.
Ushindi huo wa Yanga umewawezesha kufikisha pointi 83 wakiwashusha watani zao Simba wenye alama 82 hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Baada ya mchezo huo dhidi ya Ruvu Shooting, Yanga imebakiwa na mechi mbili mkononi huku Simba ikiwa na mechi tano.
Ruvu Shooting walijaribu kufanya mashambulizi ya kusawazisha bao hilo kupitia kwa Emmanuel Martin ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Yanga, lakini mashuti yake yaliishia kwenye miguu ya mwa gorikipa, Klaus Kindoki.
Kwa upande wa Yanga nao hawakuwa nyuma ambapo Heritier Makambo alipaisha mashuti mara mbili akiwa ndani ya 18.
Pia Soma
- Azam yajitoa rasmi mbio za ubingwa Ligi Kuu, ni vita Simba na Yanga
- Makambo azua hofu Yanga kuishusha daraja Ruvu Shooting
- Agrey Morris, Meddie Kagere chupuchupu wazichape uwanjani
Ninja alipewa kadi hiyo baada ya kumchezea rafu straika Ruvu, Emmanuel Martin aliyekuwa kwenye harakati za kupeleka mashambulizi kwenye lango lao, huku Yondan akapata adhabu hiyo kwa kosa la kuupigiza mpira chini kwa hasira.