Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaipa shavu Taifa Stars

47877 Yanga+pic

Thu, 21 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka mashabiki wake na Watanzania kwa ujumla kuweka pembeni itikadi za kishabiki na kuishangilia timu ya taifa 'Taifa Stars' itakapoumana na Uganda Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omary Kaya alisema imefika wakati kwa Watanzania kutambua thamani ya timu inayowakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.

"Hili jambo ni letu. Tuachane na yale mambo ya kusema timu hii imejaza wachezaji wa klabu fulani au haina wachezaji wa timu fulani na badala yake tuungane pamoja na kuishangilia timu ya taifa.

“Hili jambo linapaswa kuwa endelevu kuwa pale timu inapowakilisha nchi, tuwe tunaiunga mkono kwa maslahi ya nchi yetu," alisema Kaya.

Naye mjumbe wa zamani wa kamati ya utendaji ya Yanga, Godson Karigo alisema timu ya taifa ni mali ya kila Mtanzania ni lazima ishangiliwe



Chanzo: mwananchi.co.tz