Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaifuata Alliance bila Balama

85993 Pic+yanga Yanga yaifuata Alliance bila Balama

Thu, 28 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Balama Mapinduzi ataukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara, dhidi ya Alliance kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya nyonga.

Balama aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 3-2.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli alisema Mapinduzi ambaye alikuwa mchezaji wa Alliance msimu uliopita, ameshindwa kuhudhuria mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Uhuru kutokana na tatizo hilo.

"Mapinduzi bado hajapona jeraha alilolipata Ijumaa hivyo hatasafiri na timu atabaki kuwa chini ya uangalizi wa daktari ili aweze kurejea kwa haraka," alisema.

Alisema Yanga ina wachezaji wengi hivyo, wanaamini pengo la wachezaji watakaokosekana litazibwa kikamilifu na timu itapata matokeo.

Chanzo: mwananchi.co.tz