Timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mataokeo hayo yameifanya Yanga kuendelea kukaa kileleni ikiwa imefikisha alama 50 ikifuatiwa na Azam FCkatika nafasi ya pili.
Mabao ya Yanga yaliwekwa wavuni na Haritier Makambo kipindi cha kwanza huku bao pekee la Mbeya City lilifungwa na Idd Seleman.
Awali wanachama na mashabiki wa Yanga mkoa wa Mbeya walipitisha bakuli kwa ajili ya kuichangia timu yao. Akizungumza na MCL Digital Katibu wa Yanga mkoa wa Mbeya, Selemani Kondo amesema wameamua kupitisha bakuri kwa ajili ya kuisaidia timu ambayo kwa sasa haiko sawa kiuchumi. " Ni kweli bakuli linalozunguka kwa mashabiki ni sisi viongozi wa mkoa tumewatuma kwa ajili ya kuisaidia timu yetu na tumeanza tangu asubuhi ninachoshukuru michango inaendelea vizuri," amesema Kondo. Timu ya Yanga inacheza leo dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Jioni hii watani zao Simba watakuwa kwenye Uwnaja wa Taifa itakapovaana na Singida United.