Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yagawa barakoa kwa wanachama kwenye mkutano

Barako Pic Data Yanga yagawa barakoa kwa wanachama kwenye mkutano

Sun, 27 Jun 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

UONGOZI wa klabu ya Yanga katika kuhakikisha kila mwanachama wa klabu yao anapata nafasi ya kuingia katika mkutano mkuu wa klabu hiyo, wameamua kutoa bure barakoa nje ya ukumbi.

Mwanaspoti ambalo limeweka kambi ndani na nje ya ukumbi wa DYCC limeshuhudia barakoa hizo zikitolewa na mmoja wa wanachama wa Yanga.

Yanga leo wanafanya mkutano mkuu wa kupitisha mabadiliko ya klabu yao baada ya awali mkutano mkuu kutofanyika.

Mwanachama huyo ambaye alikuwa anagawa barakoa hizo alikuwa akisikika anasema barakoa hizi ni bure.

"Barakoa ni bure kwa udhamini wa GSM, Azam na Afya ukiona mtu anauza huyo ni mwizi," alisikika mwanachama huyo.

WANACHAMA WAHAKIKIWA

Wakati wanachama wakiwa wanapewa barakoa hizo, walikuwa wanapita pembeni na kwenda kuhakikiwa.

Kila mwanachama ambaye amefika katika ukumbi wa DYCC ilikuwa ni lazima kujihakiki na ukifika mlangoni wapo watu maalum ambao wanakagua kadi yako na kukuruhusu kuingia ndani.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz