Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaendeleza ubabe kwa Kagera Sugar

28839 Matokeo+pic TanzaniaWeb

Mon, 26 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kagera. Timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya  Kagera Sugar mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Mabao ya Yanga, yaliwekwa wavuni na Heritier Makambo dakika ya 21 huku Raphael Daud akiweka wavunibao la pili dakika ya 74.  Huo ni mchezo wa pili wa ugenini Yanga wakiibuka na ushindi.

Makambo ndiye alianza kuiandikia bao Yanga dakika ya 21,kisha Ramadhan Kapera kuisawazishia Kagera Sugar kwa penalti dakika ya 31 na kufikisha mabao manne katika msimu huu. Yanga watajilaumu kwa nafasi waliyokosa kupitia kwa Matheo Anthony,huku Kagera Sugar wakijilaumu kupitia kwa Christopher Edward.



Chanzo: mwananchi.co.tz