Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yacharazwa, Makambo ashindwa kuwasha mitambo

14642 YANGA+PIC TanzaniaWeb

Thu, 30 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigali. Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kwa mara ya kwanza ameiongoza dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika huku timu hiyo ikihitimisha mechi zake kwa kufungwa bao 1-0.

Mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyamirambo, umeiwezesha Rayon Sports kusonga mbele na sasa itaungana na USM Alger iliyoifunga Gor Mahia mabao 2-1 jana.

USM Alger imefikisha pointi 11 wakati Rayon ina tisa. Gor Mahia imemaliza ikiwa na pointi nane na Yanga pointi nne kutoka Kundi D.

Kocha Zahera

Kocha huyo kutoka DR Congo alikuwa kwenye benchi baada ya kufikisha takribani miezi mitano ya kuisimamia akiwa jukwaani.

Tangu alipoanza kuinoa Yanga, Zahera hakuwa akikaa kwenye benchi la ufundi na jukumu la kuiongoza timu hiyo lilikuwa chini ya kocha msaidizi Noel Mwandila.

Uwepo wa Zahera ulionekana kuipa kitu cha ziada Yanga kwa kuwa ilionyesha kiwango bora kwa kuwabana wenyeji na kutengeneza nafasi za mabao ambazo laiti ingetumia vizuri ingepata ushindi.

Yanga iliyocheza bila ya nyota wake kadhaa wakiwemo Juma Abdul na Papy Tshishimbi, ilionyesha kiwango bora hasa kipindi cha kwanza ambacho ilimiliki mpira kwa kupigiana pasi nyingi tofauti na wenyeji ambao walikuwa wakisaka matokeo zaidi.

Hata hivyo mvua iliyonyesha jana hapa Kigali, ilisababisha eneo la kuchezea kujaa maji hatua iliyowapa wakati mgumu Yanga kupenya safu ya ulinzi ya Rayon Sports kwa kuwa baadhi ya pasi zilitibuliwa na maji na kuwapa urahisi mabeki wa wapinzani wao kuondosha hatari hizo.

Pamoja na kiwango cha Yanga, safu yake ya ulinzi ilipata wakati mgumu kumdhibiti mshambuliaji Caleb Bebinyimana ambaye aliwasumbua mara kwa mara, Kelvin Yondani na Andrew Vincent.

Ni mshambuliaji huyo ambaye ndiye aliyefunga bao pekee la Rayon Sports kwenye mchezo wa jana alilokwamisha wavuni dakika ya 12 akitumia vyema uzembe safu ya ulinzi ya Yanga iliyoshindwa kumdhibiti kabla ya kumchambua kipa Benno Kakolanya.

Chanzo: mwananchi.co.tz