Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaapa kulipa kisasi kwa Mbao FC

20693 PIC+YANGA TanzaniaWeb

Thu, 4 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

KLABU ya Yanga imetaja viingilio vitakavyotumika katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbao unaotarajiwa kuchezwa Jumapili, ambapo kiingilio cha chini ni Sh 5,000 na cha juu Sh 15,000.

Akizungumza Dar es Salaam Jana, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas alisema Sh 5,000 kitatumika katika viti vya machungwa, kijani na bluu ili kutoa fursa kwa mashabiki wengi kujitokeza kuishangilia timu hiyo.

Pia, alisema Sh 10,000 ni kwa ajili ya VIP B na C huku Sh 15,000 ikiwa ni VIP A na wakati huo huo, akihimiza mashabiki kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuishangilia timu yao kama walivyofanya katika mchezo uliopita dhidi ya Simba.

“Tunatambua mchango na thamani ya mashabiki wetu ndio maana tumeweka kiingilio kidogo kwa viti vingi ili washiriki kikamilifu katika mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa saa moja usiku katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam,”alisema.

Kuelekea katika mchezo huo, Ten alisema maandalizi yanakwenda vizuri, wachezaji wote wapo fiti kwaajili ya mchezo isipokuwa Juma Mahadhi ambaye bado anasumbuliwa na majeraha ya goti.

Chanzo: mwananchi.co.tz