Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaanza kibabe Kombe la Mapinduzi

34731 Yanga+pic Tanzania Web Photo

Fri, 4 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bao pekee lililofungwa na Shaban Mohamed limeifanya Yanga kuongoza kundi B ambalo lina wapinzani wao Azam watakaokutana nao keshokutwa.

Azam jana wao walitoka sare ya bao moja dhidi ya Jamhuri wakati Yanga wameifunga KVZ dakika ya 78.

Katika mchezo huo ulioonekana kuwa na upinzani mkubwa kila upande ulifanya mabadiliko ili kupata matokeo mazuri ambapo kocha wa Yanga Noel Mwandila alimtoa Mateo Anthony aliyesababisha bao hilo.

Kocha wa KVZ, Sheikha Rashid yeye alifanya mabadiliko ya wachezaji watatu Othman Ali, Salum Maulid, na Mohamed Maulid ambao nafasi zao zilichukuliwa na Raphael Mapunda, Feisal Lucas na Masoud Masoud.

Mwamuzi wa mchezo huo Mfaume Ali katika vipindi vyote viwili vya mchezo huo alitoa kadi mbili za njano kwa kucheza rafu ambapo kadi moja ilikwenda kwa Said Juma wa Yanga na Saleh Nasoro wa KVZ.

Yanga sasa itakutana na Azam kucheza mechi yao ya pili ya kundi B ikiwa inaongoza kundi hilo



Chanzo: mwananchi.co.tz