Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wavuka maji kusaka makali ya Rollers

70216 Yangayanga+pic

Wed, 7 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

JESHI  zima la Yanga wakiwamo wale waliokuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars', limeondoka asubuhi hii kwenda Zanzibar kuweka kambi ya siku tatu ambapo ikiwa huko itacheza mechi mbili ili kuwanoa makali ya kuwavaa Township Rollers ya Botswana.george lwandamina,

Yanga na Township zinatarajiwa kuvaana Jumamosi hii Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam katika mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 2-1 ilichopewa walipokutana mwaka jana.

Katika mechi hiyo ya raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa kwa msimu huo, Yanga ilikuwa chini ya Mzambia George Lwandamina na kulala nyumbani 2-1 kisha kwenda kulazimishwa suluhu ugenini mjini Gaborone na kutupwa kwenye Kombe la Shirikiso Afrika.

Yanga kwenye hatua hiyo ya play-off ya Kombe la Shirikisho walifanya kweli kwa kuizamia Welaita Dicha nya Ethiopia na kutinga makundi ikiwa ni mara yao ya pili baada ya kufanya hivyo kwenye michuano hiyo mwaka 2016.

Kwa kutaka kutorudia makosa mbele ya Township Kocha Mwinyi Zahera ameomba kambi ya siku chache Zanzibar na kucheza mechi mbili za kujipima nguvu dhidi ya Mlandege itakayopigwa usiku wa kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Amaan, ili kunoa makali yake.

Mechi yao ya pili itakuwa dhidi ya Malindi ambayo inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika mchezo ambao nao utapigwa usiku kwenye uwanja huo wa Amaan kabla ya Ijumaa timu hiyo kurejea tayari kuwapokea Township ambayo inatarajiwa kuwasilia nchini Alhamisi.

Yanga ikiwa na majembe yake yote akiwamo Paul Godfrey, Metacha Mnata, Feisal Salum sambamba na nyota wapya waliosajiliwa hivi karibuni walikuwa sehemu ya msafara wa kikosi hicho, huku nyota hao wakionekana kuwa na mzuka kama wote.

Baadhi ya nyota wapya waliokuwa kwenye msafara huo ni Juma Balinya, David Molinga 'Ndama' a.k.a  Falcao, Sadney Urikhob, Issa Bigirimana na Patrick Sibomana na timu hiyo iliodnoka kwa boti Bandari ya Dar es Salaam saa 3 asubuhi ya leo.

Chanzo: mwananchi.co.tz