Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wamepoteza point ya 17 VPL msimu huu 2017/2018 leo

1472 1210 660x400

Thu, 18 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Baada ya Ligi Kuu Tanzania bara kusimama kwa kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi 2018, leo January 17 2018 Ligi Kuu iliendelea kwa Bingwa mtetezi Yanga kuwakaribisha Mwadui FC ya Shinyanga.



Yanga waliingia uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kucheza game yake ya 13 na Mwadui FC lakini bahati haikuwa kwa Yanga na wameambulia point moja baada ya game yao kumalizika kwa sare tasa 0-0, matokeo ambayo yamewafanya kukaa nafasi ya tano katika msimamo wa VPL wakati Mwadui FC  wakiwa nafasi ya 9.

Huu unakuwa ni mchezo wa saba kwa Yanga kutoka sare wakiwa wameshinda game tano na kupoteza game moja pekee, ukijumlisha point 14 walizopoteza kwa kutoka sare na point tatu walizopoteza kwa kufungwa na Mbao FC wanakuwa wameshindwa jumla wameshindwa kuvuna point 17 msimu huu.

TFF imetangaza kumfungia Obrey Chirwa wa Yanga

Chanzo: millardayo.com