Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga vs Njombe Mji, Obrey Chirwa kapiga hat-trick huko!!!

2746 31 660x400

Wed, 7 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Dar es salaam Young Africans leo walikuwa nyumbani katika uwanja wao wa Uhuru kuikaribisha timu ya Njombe Mji kutoka Njombe.



Yanga wakiwa nyumbani wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 4-0 na kufanikiwa kuvuna point zote tatu, magoli ya Yanga yalifungwa na Obrey Chirwa aliyefunga hat-trick dakika ya 46, 64,87 na Emmanuel Martin aliyefunga dakika ya 69 .



Ushindi huo sasa unaifanya Yanga kutimiza jumla ya point 34 na kushika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu nyuma ya Simba inayoongoza kwa point 38 lakini Yanga ameizidi Simba na Azam FC zitakazocheza kesho Uwanja wa Taifa amezizidi mchezo mmoja.



Msimamo wa VPL baada ya game za leo



VIDEO: Okwi amedaiwa kupoteza fahamu uwanjani baada ya kupigwa kiwiko

Chanzo: millardayo.com