Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga vibonde wa Azam

35004 Azaaam Azam dhidi ya Yanga

Mon, 7 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zanzibar. Ushindi wa bao 3-0 walioupata Azam dhidi ya Yanga umeishusha hadi nafasi ya pili kwenye kundi B la mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

Mechi hiyo imechezwa usiku wa leo Jumamosi uwanja wa Amaan

Mabao ya Azam yalifungwa na Obrey Chirwa aliyepachika mabao mawili na Enock Atta.

Mabao mawili yalifungwa kipindi cha kwanza wakati bao la tatu Chirwa lilifungwa dakika ya 60.

Ushindi huu wa Azam unawapandisha hadi nafasi ya kwanza kundi B wakiwa na pointi nne wakati Yanga wao wanashika nafasi ya pili kwa pointi tatu.

Kocha wa Azam Hans Pluijm alifanya mabadiliko kipindi cha pili ambapo aliwatoa Joseph Mahundi, Tafadzwa Kutinyu, Chirwa na Atta ambapo nafasi zao zilichukuliwa na Ramadhan Singano, Salmin Hoza, Donald Ngoma na Iddi Kipangwile.

Kocha wa Yanga, Noel Mwandila naye alifanya mabadiliko kwa kumtoa Gustafa Saimon aliyeumia na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ilichukuliwa na Faraji Kilaza.



Chanzo: mwananchi.co.tz