Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga uwanjani tena bila Zahera

68392 Pic+zahera

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

YANGA inatarajiwa kucheza mchezo wa nne wa kirafiki kesho Jumamosi dhidi ya mabingwa wa Burundi, Aigle Noir.

Ikiwa kambini mkoani Morogoro, Yanga itacheza mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya kwanza kukutana na timu kutoka nje ya nchi huku ujio wa Kocha Mkuu wake, Mwinyi Zahera ukiwa bado utata.

Zahera, ambaye alikuwa na timu ya Taifa ya DR Congo kwenye Fainali za Afcon kule Misri, bado hajarejea nchini wakati kikosi chake kikiendelea kujifua kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara chini ya Noel Mwandila.

Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema bado Mwandila anahitaji mechi za kirafiki kukipima kikosi chake.

Saleh amesema mchezo huo utapigwa uwanja wa Highland Park ambao Yanga inautumia kwa mazoezi ambapo mabingwa hao tayari wametua Morogoro.

Hafidh amesema kuna uwezekano mkubwa wa Yanga kucheza dhidi ya Mawenzi Market inayoshiriki ligi daraja la pili msimu ujao.

Pia Soma

Noir tangu watua nchini wamecheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya Namungo FC, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar walipoteza mbili na kutoa sare moja.

Timu hiyo awali imefungwa na Namungo kisha kupokea tena kipigo kutoka Kagera zote wakifungwa mabao 3-0 kila mmoja kisha kutoa suluhu ya bao 2-2 dhidi ya Mtibwa Sugar

Chanzo: mwananchi.co.tz