Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga sasa ya kisasi

C67df87c0be1bf603a17577a36b75ce1 Yanga sasa ya kisasi

Mon, 28 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS Mstaafu wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete amewapongeza Wanachama wa klabu ya soka ya Yanga kwa kupitisha mabadiliko ya Katiba yatakayowawezesha kubali mfumo wa uendeshaji wa timu hiyo.

Wanachama 1770 walihudhuria katika mkutano huo na wote kwa pamoja kupitisha mabadiliko hayo baada ya kuridishwa na mchakato uliofanywa kwa muda mrefu wa kuipeleka timu hiyo katika uendeshwaji mpya.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi, alianza kwa kuwapongeza viongozi wa timu hiyo kwa uwazi waliokuwa nao katika masuala ya kifedha na ukaguzi jambo ambalo limekuwa tatizo kwenye taasisi nyingi nchini.

Dk Kikwete alisema wanachama wamefanya uamuzi sahihi wa kukubali muundo uliopendekezwa, ambao utapelekea klabu kuendelea kubaki mikononi mwao

"Mwekezaji asigeuzwe kuwa mmiliki wa klabu hii ni klabu ya wanachama, mwekezaji anakuja kujumuika na wenye klabu yao kusogeza klabu mbele kibiashara na sio kujimilikishia klabu, nilichovutiwa na Yanga mabadiliko haya ni shirikishi, yamejadiliwa na maoni yamepokelewa.”

Kiongozi huyo alisema baada ya mabadiliko hayo, hatarajii kuona vikundi vya watu wakipingana huko nje.

Baada ya kushirikishwa kikamilifu katika kila hatua ambayo imepitiwa mpaka kufikia hatua hiyo, ikiwepo majadiliano kabla mchakato huo haujapitishwa jana.

“Mashabiki wa Yanga wakosoe kwa nia ya kujenga na sio kukosoa kwa lengo la kukomoa. Msiache kusema kwenye mkutano mkuu halafu mnaenda kulalamika vijeweni. Huo ni usengenyaji. Watu wa namna hii waambieni, acheni uchimvi. Usianzishe ligi mtaani mnabomoa klabu yenu," alisema.

Aidha, Dk Kikwete pia ameutaka uongozi wa Yanga kuwa makini katika kuboresha eneo la benchi la ufundi kwa kutafuta kocha mzuri pamoja na wachezaji wenye ubora ili kuebuka mabadiliko ya mara kwa mara ya timu ambayo kiufundi haya afya kwa maendeleo ya Yanga.

Alisema subra ni jambo la msingi katika kujenga timu ili kupata mafanikio siku za baadaye na kuwataka wanachama kuwa wavumilivu wanapokuwa na kocha mpya au wachezaji wapya lengo ni kuwapa muda kuzoea mazingira.

"Naamini kama mtakuwa na makocha wazuri na wachezaji wenye viwango kisha mkawalipa vizuri na kwa wakati itapunguza klabu kutegemea zaidi Kamati za Ufundi kuliko benchi la ufundi, klabu ikiendekeza sana Kamati za Ufundi haiwezi kupiga hatua inadumaa."

Kiongozi huyo alimalizia kwa kusema Yanga ni timu yake anayoipenda sana inapofungwa anaumia na inaposhinda anafurahi sana na anaamini Jumamosi inayokuja itashinda mechi dhidi ya watani zao wa jadi Simba mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Dk Mshindo Msolla aliwashukuru wanachama kwa kuridhia na kupitisha mabadiliko ya Katiba hiyo ambayo mchakato wake uliwategemea wao zaidi katika kupata maoni yao ili kufikia hatua hiyo.

Aidha Dk Msolla kupitia mkutano huo alitangaza kuwarudisha kundini wajumbe wao watatu wa Kamati ya Utendaji kutokana na makosa mbalimbali na baada ya uchunguzi umegundua hawakuwa na makosa na wapohuru kuendelea na majukumu yao ya kuiongoza Yanga.

Wajumbe hao ni Rojas Gumbo, Salum Rupia na Frank Kamugisha pia Dk Msolla alitangaza majina matano ya wajumbe wanaounda Baraza jipya la Wadhamini wa klabu hiyo, ambao ni George Mkuchika, Geofrey Mwambe na Abbas Tarimba

GSM YAAHIDI MAKUBWA

Injinia Hesri Said wa GSM aliyezungumza kwa niaba ya Rais wa Kampuni hiyo alisema wataendelea kuisaidia Yanga kuhakikisha inakuwa timu yenye ushindani na mafanikio Afrika.

Hersi alisema wataendelea kuipigania Yanga bila ya kujali watakuwa miongoni mwa wawekezaji au la.

MANJI ATOA NENO

Katika mkutano huo alikuwepo Mwenyekiti wazamani wa Yanga, Yusufu Manji alisema anajisikia faraja kurejea nyumbani baada ya muda mrefu kupita akiwa nje ya nchi.

Alisema aliacha moyo wake Jangwani na amefurahi kupewa mwaliko wa kushiriki mkutano huo mkuu jana.

Ujio wa Manji uliibua shangwe na nderemo kutoka kwa wanachama ikiwa ni takribani miaka minne imepita tangu aliposhiriki harakati za Yanga.

KATIBU TFF AZOMEWA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Wanachama wa klabu ya Yanga, walimzomea Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred wakidai kuwa taasisi hiyo haiwatendei haki katika mambo mengi ya kimaamuzi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz