Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga sasa haitaki mbeleko kimataifa

KIPA Yanga sasa haitaki mbeleko kimataifa

Thu, 24 Jun 2021 Chanzo: ippmedia.com

Yanga imewasili salama Tabora, kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, utakaochezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Kikosi cha Yanga kimeenda mkoani humo na silaha zake kamili na kujumuisha kikosini kipa, Godfrey Magaigwa akitokea katika Kikosi B cha timu hiyo, ambaye aliibuka kuwa mlinda mlango bora wa ligi ya vijana iliyofikia tamati mwishoni mwa wiki iliyopita, Uwanja wa Azam Complex kwa Mtibwa Sugar U-20 kuibuka mabingwa.

Akizungumza na gazeti hili jijini jana, Kocha wa Makipa wa Yanga, Razak Siwa, alisema wamejipanga vizuri na wachezaji wao wako tayari kwa ajili ya kutafuta ushindi kwenye mchezo huo muhimu dhidi ya Biashara United.

"Hatutaki kupoteza katika mchezo huu, lazima tupambane kutafuta matokeo mazuri, malengo yetu ni kushiriki michuano ya kimataifa kwa nguvu zetu, tunahitaji matokeo ya ushindi katika mchezo huu kwa ajili ya fainali," alisema Siwa.

Bingwa wa michuano ya Kombe la FA, ataiwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo: ippmedia.com