Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga na Simba waingiza Sh500 milioni Uwanja wa Taifa

98458 Pic+mapato Yanga na Simba waingiza Sh500 milioni Uwanja wa Taifa

Mon, 9 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mashabiki wa Simba pamoja na timu yao kufungwa bao 1-0 wamefanikiwa kuichangia Yanga mapato ya zaidi ya Sh 545milioni katika mchezo huo wa watani wa jadi uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ulioshuhudiwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli na Rais wa CAF, Ahmed Ahmed na Rais wa TFF, Wallace Karia pamoja na mashabiki 59,325 waliojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60000 waliokaa.

Mshambuliaji Bernard Morrison alikuwa shujaa wa Yanga kwa kufunga bao pekee kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja wavuni na kumuacha kipa wa Simba, Aishi Manula akiruka bila matumani katika dakika 44 ya kipindi cha kwanza.

Pamoja na Yanga kushinda sehemu kubwa ya mashabiki waliojitokeza katika uwanjani hapo walikuwa wa Simba.

Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo leo alitangaza mapato yaliyopatikana kwa mashabiki 59,325 ni zaidi ya Sh545 milioni.

Mapato hayo Yanga wenyeji wa mchezo huo wanataraji kupata zaidi ya Sh200 milioni hiyo ni baada ya makato mbalimbali pamoja na kodi.

Pia Soma

Advertisement
Wakati mchezo jana mashabiki 59,325 waliingia uwanjani katika mchezo wa kwanza uliopigwa Januari 4, 2020 na kumaliza kwa sare 2-2, ambao Simba alikuwa mwenyeji ulitazamwa na mashabiki 57,000 na kuingiza Sh 539milioni.

Chanzo: mwananchi.co.tz