Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga mambo magumu, hesabu zote kumalizia Misri

81955 Pic+yanga+zz Yanga mambo magumu, hesabu zote kumalizia Misri

Mon, 28 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Yanga imeweka njia panda nafasi yake ya kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Pyramids FC.

Katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, Pyramids ilipata mabao yale kupitia Erick Traore dakika 43 na Mohammed Farouk dakika ya 65, kabla ya Patrick Tshitshimbi kufunga la kufutia machozi kwa Yanga katika dakika ya 88.

Kwa matokeo hayo Yanga sasa watalazimika kushinda 2-0 au ushindi wa zaidi ya mabao 3 ili kusonga mbele kwa mashindano hayo Afrika wiki ijayo.

Yanga watakwenda Misri watamkosa beki wake Kelvin Yondani aliyepata kadi nyekundu baada ya kupewa kadi mbili za njano.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila alisema wachezaji wake walicheza kwa presha kubwa kipindi cha kwanza ndio maana wakaruhusu bao, lakini cha pili walifanya uzembe wa kukaba, ameongeza watapambana kwa mechi ijayo.

"Mechi ilikuwa ngumu, Pyramids walichezea zaidi mpira kipindi cha kwanza, lakini sisi tukawaweza cha pili, ni uzembe tu na presha ikapelekea tukafungwa mabao hayo, pado tunahitaji kusonga mbele, tutapambana," alisema Mwandila.

Pia Soma

Advertisement
Kocha wa Pyramids FC, Sebastien Desabre alisema licha ya uwanja wa kuwa sio rafiki kwa upande wao, lakini wametumia vizuri nafasi walizopata kufunga mabao.

Chanzo: mwananchi.co.tz