Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kutoidharau Mwadui

Fe5396b0c48ea5fee540d6c0f5f8e0ed.jpeg Yanga kutoidharau Mwadui

Mon, 24 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

LICHA ya kuwa Mwadui ndio timu ya kwanza kushuka daraja katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amesema ataingia na tahadhari kubwa katika mchezo wa hatua ya robo fainali ugenini dhidi ya timu hiyo, mtanange utakaochezwa katika Uwanja wa CCM Kambarage, mkoani Shinyanga.

Yanga itashuka katika Uwanja wa CCM Kambarage ikiwa na kumbukumbu nzuri baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 katika mchezo wa Ligi kuu ya Tanzania Bara.

Yanga imetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, wakati Mwadui FC waliwaondosha Coastal Union kwa mabao 2-0 katika Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.

Akizungumza na gazeti hili jana, Nabi alisema huo ni mchezo muhimu kwake na kikosi chake kwani utatoa nafasi ya kuingia hatua ya nusu fainali na kulikaribia taji la Shirikisho la Azam ambalo linatoa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

“Naamini utakuwa mchezo mgumu na wenye upinzani, kwani kila timu itakuwa ikiwania nafasi ya kuingia nusu fainali japokuwa wenyeji Mwadui watakuwa nyumbani mbele ya mashabiki wao, hivyo tunapaswa kuwa makini sana ili tuweze kutimiza malengo yetu.”

“Tunapaswa kuongeza umakini hasa sehemu ya ulinzi tusiruhusu bao na nafasi ya ushambuliaji watumie kila nafasi tutakazo pata ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali,” alisema Nabi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz