Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kumtambulisha straika mpya Ukumbini

62808 YANGA1+PIC

Sat, 15 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MOJA ya sapraizi kubwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo Jumamosi ni Yanga kumtambulisha straika mpya.

Taarifa ambazo zimepatikana ni kwamba Yanga itamtambulisha mchezaji huyo ambaye atakuwa mchezaji wa nane wa kigeni kusajiliwa na timu hiyo.

Hata hivyo viongozi wa Yanga wamekuwa wazito kutoa jina la mchezaji huyo wakitaka kuwapa sapraizi mashabiki na wanachama wao ukumbini.

Uchunguzi wa Mwanaspoti Online umebaini kwamba kuna uwezekano wa asilimia 100 Yanga inatambulisha mshambuliaji Juma Balinya raia wa Uganda.

Balinya aliibuka mfungaji bora msimu uliopita katika Ligi Kuu ya Uganda akifunga jumla ya mabao yasiyopungua 21.

Inaelezwa kwamba mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga.

Kama Yanga itakuwa imemnasa Balinya kuna uwezekano ikawa imeipiga bao Simba ambao alikuwa mmoja ya wachezaji waliotajwa kuhitajiwa na timu hiyo

Chanzo: mwananchi.co.tz