Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuliamsha kweupee

69382 Yanga+picha

Thu, 1 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

YANGA kumenoga! Baada ya kujifua kwa wiki mbili mjini Morogoro, Kikosi cha Yanga kimepanga kurejea kesho Ijumaa mchana kweupe kisha fasta kupiga tizi kujiandaa na mechi yao ya kimataifa dhidi ya Kariobang Sharks ya Kenya itakayopigwa siku ya Kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Mabosi wa klabu hiyo wamejivunia kambi hiyo ya mjini Morogoro, wakidai imesaidia kwa kikubwa vijana wao kunoa makali na sasa imefika wakati wa kuwasha moto kwenye michuano ya ndani na ile ya kimataifa wakishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga Hamad Islam amesema kwamba kesho mchana kikosi chao kitaanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam.

Islam ambaye alikuwa akiongoza usimamizi wa kambi hiyo sambamba na mjumbe mwenzake Mhandisi Bahati Mwaseba amesema kambi yao imekuwa na mafanikio makubwa.

Amesema wakiwa Morogoro wachezaji na makocha wamekuwa katika utulivu mkubwa wa kupata maandalizi ya kutosha katika kujiandaa na msimu mpya.

Kiongozi huyo amesema kuwa uongozi wao umeridhika na kazi iliyokuwa inafanyika katika maandalizi hayo ambapo sasa wanarejea jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi.

Aidha Islam licha ya kuwapongeza wanachama na mashabiki wa timu hiyo mkoani humo amewataka mashabiki hao kusafiri kwa wingi kwenda kuungana na wenzao katika mchezo wa Jumapili Agosti 4 dhidi ya Kariobang.

Chanzo: mwananchi.co.tz