Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kujipanga ujipanga upya

9714b9451a579fc4303e70eab8ddc98d Yanga kujipanga ujipanga upya

Mon, 12 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SARE ya bao 1-1 iliyopata Yanga dhidi ya KMC imeongeza presha kwa mashabiki wa timu hiyo na kuanza kuwanyooshe vidole wachezaji wao, lakini Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo, Juma Mwambusi amesema ameyachukua matokeo hayo kama kipimo cha michezo iliyosalia ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa juzi, ulikuwa wa 24 kwa Yanga ambao wamefikisha jumla ya pointi 51 katika msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Hiyo ilikuwa sare ya pili mfululizo tangu duru la pili la ligi hiyo lianze, ya kwanza ikiwa ni ile ya Polisi Tanzania na kuzidi kutoa nafuu kwa Azam FC inayoshika nafasi ya pili pamoja na watani wao wa jadi klabu ya Simba inayoshika nafasi ya tatu huku ikiwa na michezo minne ya viporo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mwambusi alisema ameona mapungufu ya kikosi chake ambayo anaenda kuyafanyia kazi kwa ajili ya kuendelea na harakati za kulisaka taji la Ligi Kuu ambalo wamelikosa kwa misimu mitatu mfululizo.

“Kama mwalimu sikutarajia kupata pointi moja katika mchezo huu, lakini KMC walikuwa na siku nzuri kazini hasa kipindi cha kwanza ndio maana walifanikiwa kupata bao la uongozi mapema.”

“Mpira una matokeo ya kikatili sana lakini hatuwezi kukata tamaa tunarudi kujipanga upya ili tusiweze kuyarudia makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita,” alisema Mwambusi.

Naye Kocha Msaidizi wa KMC, Habib Kondo alisema malengo yao yalikuwa kuondoka na pointi tatu na kulipa kisasi katika mchezo huo ku

Chanzo: www.habarileo.co.tz