Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kujenga viwanja vitatu eneo la Makonda

63798 Pic+makonda

Sat, 22 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

UONGOZI wa Yanga umepanga kujenga viwanja vitatu vya mpira kwenye eneo walilopewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mbali na viwanja hivyo, pia kwenye eneo hilo kutajengwa kituo cha mcho wa soka, hoteli na nyumba za wachezaji wa kigeni.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji ya Yanga, Lucas Mashauri ameweka wazi mipango hiyo muda mfupi baada ya kukabidhiwa eneo hilo la ekari saba lililopo Kibada nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Alisema mpango wa klabu ni kuijenga uwanja mkubwa wa soka na viwanja vingine viwili vidogo kwenye eneo hilo walilolipa jina la Yanga Sports Club Complex.

"Mchakato wa ujenzi utaanza wakati wowote kuanzia sasa," alisema Mashauri.

Chanzo: mwananchi.co.tz