Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kamwene! Yatinga kibabe nusu fainali FA

49584 YANGA+PIC

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kipa Klause Kindoki ameibuka shujaa baada ya kupangua penalti mbili za Alliance FC na kuipeleka Yanga hadi nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.

Katika mchezo huo uliofanyika leo Jumamosi Kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, Yanga imeibuka na ushindi wa penalti 4-3 baaada ya sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Yanga ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Heritier Makambo dakika ya 38

kwa shuti kali na mpira huo kugonga mwamba kisha kutinga wavuni, akimalizia pasi safi kutoka kwa Pius Buswita.

Bao hilo lilionekana kama la maajabu kwani mpira huo baada ya kuingia wavuni ulichana nyavu na kutoka nje.

Baada ya kuingia kwa bao hilo,Makambo alishangilia kwa kucheza sebeneĀ  kuanzia nje mpaka katikati ya uwanja akionekana mwenye furaha.

Alliance ambao dakika 30 za kipindi cha kwanza walicheza vizuri na kuwabana vilivyo Yanga walijikuta wakipoteabna dakika 15 za mwisho za kipindi hicho baada ya watoto wa Jangwani kuamka na kucheza soka safi.

Katika penalti hizo Yanga walifunga kupitia kwa Paul Godfrey,Thaban Kamusoko, Haruna Moshi 'Boban' Deus Kaseke huku Kelvin Yondani na Mrisho Ngassa wakikosa.

Waliofunga kwa upande wa Alliance niĀ  Joseph James,Geofrey Luseke na Sameer Vincent wakati Dickson Ambundo Siraji Juma walikosa.

Kwa ushindi huo, Yanga inakwenda kukutana na Lipuli FC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali.



Chanzo: mwananchi.co.tz