Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga hao kileleni!

18122 Pic+yanga TanzaniaWeb

Wed, 19 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Yanga SC  itacheza usiku wa leo Jumatano saa 1:00, mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union  na habari nzuri kwao ni kwamba, wana nafasi kubwa ya kuongoza msimamo.

Yanga iliyocheza mechi mbili na kushinda zote, endapo wataifunga Coastal Union yenye mchezaji maarufu kwenye Bongo Fleva, Ally Kiba itafikisha pointi tisa, lakini presha yao itakuwa kwa timu za JKT Tanzania, Mtibwa Sugar na Azam FC.

Yanga inacheza mchezo huo huku wakiziombea mabaya JKT Tanzania ambao ndio vinara wa ligi wakiwa na pointi nane, wanacheza na Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex, endapo  watashinda watafikisha pointi 11 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine hadi michezo ya raundi ya sita.

Pia, Wakata miwa wa Mtibwa Sugar wenye pointi saba ambao watakuwa ugenini Uwanja wa Nangwanda Sijaona kukipiga na Ndanda FC nao wakishinda watafikisha pointi 10, sawa na Azam FC watakaokuwa  Uwanja wa Kumbukumbu ya Mandela kucheza na Biashara United.

Mechi nyingine zitakazochezwa leo lakini hazina madhara kwa Yanga ni Lipuli FC dhidi ta Alliance FC Uwanja wa Samora na

Mbeya City watakipiga na Ruvu Shooting  Uwanja wa Sokoine.

MECHI ZA KESHO ALHAMISI

Mbao FC na Simba Uwanja wa CCM Kirumba

Tanzania Prisons na Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine

African Lyon na Singida United Uwanja wa Uhuru

 

Chanzo: mwananchi.co.tz