Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga haikamatiki Ligi Kuu, yaichapa Lyon 1-0

32610 Kindoki+pic Tanzania Web Photo

Thu, 20 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dara es Salaam. Timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya  ya African Lyon mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Alhamisi.

Bao la Yanga liliwekwa wavuni na Abdallah Shaibu kipindi cha pili katika dakika ya 64' na kuifanya timu hiyo ya Mtaaa wa Jangwani kuvuna alama tatu na kuendelea kujiimarisha kileleni wakiwa na pointi 47.

Awali, katika kipindi cha kwanza mpira ulianza kwa timu zote zikicheza kwa kufanya mashambulizi ya kushtukiza huku  wakionekana kutaka kupata goli la mapema ili kutangulia kutafuta ushindi.

Licha mchezo kuwa na spidi ya hali ya juu hakuna ambaye aliweza kuona goli la mwenzake ndani ya dakika 45 za kwanza katika mchezo huo.

Uwanja ulionekana kuwa kikwazo kwa timu zote baada ya kukosekana ufundi katika kuwea mpira chini badala yake walikuwa wakitumia mipira mirefu kupeleka mashambulizi.

Dakika 16 Yanga ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Jaffary Mohammed aliyepata maumivu na kuingia Deus Kaseke.

Yanga ilifanya shambulizi langoni mwa Africa Lyon, baada ya dakika 32 mshambuliaji Amis Tambwe alikosa goli baada ya kupiga kichwa na mpira kutoka nje kupitia  faulo iliyopigwa na Gadiel Michael.

Dakika 38 Ramadhan Kabwili alishindwa kuendelea na mpira baada ya kulala chini akishilia kupata maumivu, lakini alipopewa huduma ya kwanza alionyesha kutoweza kuendelea na nafasi yake ilichukuliwa na Klaus Kindoki.

Amis Tambwe alionekana kutaka kufunga goli la mapema baada yakuongeza spidi ya mashambulizi na dakika 44 alinyoosha shuti kali akiwa nje ya 18 hata hivyo umakini wa kipa Doglas Kasebo aliudaka mpira huo kwa makini.

Dakika 46 Gadiel Michael alipewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Jabir Stima ambaye alikuwa katika halakati za kuitafutia goli timu yake.

Kipa wa Lyon aliogeuka kuwa nguzo muhimu ya Lyon baada ya ya dakika 53 kuokoa mchomo wa Ibrahim Ajib, alipopiga shuti la juu juu na kutaka kuingia wavuni hata hivyo aliupangua mpira huo.

Yanga walikuwa wakitumia upande wa kulia kupeleka mashambulizi, hasa wakimtumia Paul Godfrey ambaye alikuwa akipiga krosi nyingi lakini hata hivyo umakini ulikuwa mdogo.

Dakika 58 Kassim Simbaulanga alipewa kadi ya njano baada ya kumfanyia faulo Paul Godfrey, upande amabo ulikuwa na kashikashi ya aina yake dhidi ya wachezaji hao.

Tambwe alitaka kuiandikia bao la kuongoza dakika 63 baada ya kupenyezewa pasi na Ibrahim Ajib na kunyoosha shuti kali lilipanguliwa na kipa Douglas Kasebo.

 Dakika 64 Yanga ilipata bao baada ya Ibrahim Ajib kupiga faulo ambayo Abdallah Shaibu ‘Ninja’ alionganisha kwa kichwa na kuwafanya Africa Lyon wawe nyuma licha ya kwamba walikuwa wakionesha kutaka bao la mapema katika mchezo huo.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz