Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga chupuchupu... yaing'oa Biashara United kwa penalti

39474 Yanga+pic Yanga chupuchupu... yaing'oa Biashara United kwa penalti

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kikosi cha Yanga kimesonga mbele kwenye mashindano ya Kombe la FA baada ya kuing'oa Biashara United ya Mara kwa jumla ya penalti 5-4, katika mchezo uliopigwa jana Alhamisi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Yanga, Matheo Antony ndiye aliyepiga penalti ya mwisho katika mchezo huo iliyokwenda moja kwa moja golini na kuwafanya mashabiki wa Yanga kuamsha furaha ya ajabu kutokana na matokeo hayo ambayo ni ya hatua ya nne na wanakwenda Lindi kucheza na Namungo FC.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Yanga walikuwa nyuma kwa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United.

Bao la Yanga lilifungwa na Amiss Tambwe ambalo lilikuwa la kusawazisha kabla ya Bishara kufunga bao la pili dakika nne kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Dakika ya 74 Makambo aliifungia Yanga bao la kusawazisha na kuzifanya timu hizo kumaliza dakika 90 wakitoka sare ya mabao 2-2 na kwenda hatua ya mikwaju.

Yanga walionekana kushambulia mara kwa mara ingawa hawaweza kutengeneza mashambulizi ya hatari zaidi.

Mashambulizi ya Yanga yalikuwa yale ya kosa kosa huku Biashara wakionekana kuimarika zaidi katika safu y ulinzi wakiongozwa na kipa wao.

Kwa upande wa Biashara ambao kipindi cha kwanza walipata mabao mawili mbali ya kushambulia mara chache kuliko Yanga lakini waliweza kutumia vizuri makosa ya wapinzani wao.

Bao la kwanza lilikuwa ni penati dakika ya kwanza ya mchezo baada ya beki Vicent Dante kupitwa na kuamua kucheza rafu.

Bao la pili lilikuwa ni makosa ya wachezaji wa Yanga kupoteza mpira kiurahisi kabla ya mabeki wao kupigwa changa na kufungwa bao la pili.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz