Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Yapangwa na Rivers United ya Nigeria

Downloads1?fit=800%2C450&ssl=1 Yanga Yapangwa na Rivers United ya Nigeria

Fri, 13 Aug 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

DROO ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2021/2022 ambayo imetoka leo inaziweka Simba na Yanga katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi kama zitachanga vyema karata zao kwenye mechi za hatua ya awali

Wawakilishi hao wa Tanzania Bara kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wamepangwa kukutana na timu ambazo zinaonekana zinaweza kupambana nazo na kuzitupa nje kama zitajipanga vizuri.

Simba ndio inaonekana kuwa na mchekea zaidi kwani yenyewe itaanzia raundi ya kwanza bila kucheza hatua ya awali na hapo itakutana na mshindi baina ya Jwaneng ya Botswana na DFC Beme ya Afrika ya Kati.

Wakati Simba ikianzia katika raundi ya kwanza na mshindi baina ya Jwaneng na DFC Beme ya Afrika ya Kati, wenzao Yanga ambao watakuwa nao katika mashindano hayo wamepangwa kuanzia nyumbani dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

Mshindi baina ya mchezo kati ya Yanga na Rivers United atakutana na mshindi wa mchezo baina ya Fasil Kenema ya Ethiopia na Al Hilal ya Sudan.

Rivers United iliyopangwa kukutana na Yanga ilianzishwa mwaka 2016 baada ya timu mbili kuungana ambazo ni Sharks na Dolphins na msimu uliopita imemaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Nigeria.

Inafundishwa na Kocha Stanley Eguma na inatumia Uwanja wa Yakubu Gowon ambao upo katika jiji la Port Harcourt lililopo kwenye jimbo la Rivers, Mashariki mwa Nigeria.

Hii ni mara ya pili kwa Rivers United kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni 2017 walipotolewa katika hatua ya kwanza na Al Merrikh ya Sudan kwa kipigo cha mabao 4-3.



 
Chanzo: globalpublishers.co.tz